JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU.​

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
​
Ikulu, Dar es Salaam Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 18 Novemba, 2016 amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Bw. Diwani Athuman kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera. Uteuzi wa Bw. Diwani Athuman unaanza mara moja.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi katika Taasisi Tano za Serikali kama ifuatavyo. Kwanza, Rais Magufuli amemteua Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jaji Joseph Sinde Warioba kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu des Sokoine cha Kilimo (SUA) Uteuzi huu umeanza tarehe 16 Novemba, 2016.

Pili, Rais Magufuli amemteua Dkt. Jones A. Kilimbe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na amemteua Bw. Sylvester M. Mabumba kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Uteuzi huu umeanza tarehe 17 Novemba, 2016 Tatu, Rais Magufuli amemteua Prof. Patrick Maktuigu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo (TEMDO). Uteuzi huu umeanza tarehe 16 Novemba, 2016.

Nne, Rais Magufuli amemteua Bw. Martin Madekwe kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi. Uteuzi huu umeanza tarehe 17 Novemba, 2016.

Tano, Rais Magufuli amemteua Prof. Raphael Tihelwa. Chibunda kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wakurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Viwaatilifu vya Kitropiki Tanzania (TPRI) Uteuzi huu umeanza tarehe 17 Novemba, 2016.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
IKULU Dar es Salaam
18 Novemba, 2016. 
 
DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: