MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) aliyejiengua na kurejea katika nafasi hiyo, Prof. Ibrahim Lipumba, amesema yupo tayari kufanyakazi na katibu mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, bali anachosubiri kwa sasa ni kumalizika kwa kesi iliyopo mahakamani.


Prof. Lipumba alitoa kauli hiyo juzi alipofanya mkutano wa ndani wa viongozi na wanachama wa CUF mkoa wa Tabora.

Alisema hana kinyongo na Maalim Seif ndiyo maana yupo tayari kuendelea kufanya naye kazi ya kukiimarisha chama chao ambacho kimeyumba kutokana na mgogoro wa uongozi ulioibuka Agosti, mwaka huu.

β€œNimekuwa nampigia simu, lakini hapokei, hatuongei naye huo ni mtihani, lakini nina imani ipo siku tutafanyakazi pamoja kujenga chama chetu,” alisema.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: