
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
SIMBA imetangaza dau la Sh milioni 240 kwa ajili ya kumrejesha
mshambuliaji Emmanuel Okwi, ambaye hadi sasa amecheza mechi nne tu
katika timu ya SonderjyskE.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, Okwi tangu ajiunge na timu hiyo ya
Denmark Julai 10 mwaka jana akitokea Simba, amecheza mechi nne za Ligi
Kuu nchini humo maarufu kama Danish Sas Ligaen na hajafunga goli hata
moja, huku akiwa na kadi moja ya njano.
Ushindani wa namba unamweka benchi baada ya kucheza mechi mbili msimu
wa mwaka jana na mbili msimu huu kati ya michezo 16 iliyochezwa kwenye
ligi hiyo kwa sasa, ikiwa inashika nafasi ya sita kwenye msimamo na
pointi zake 23, huku timu kinara ikiwa ni FC Copenhagen yenye pointi 38,
ikifuatiwa na Brondby 32, Midtjyland 29, Randers 29 na Lyngby 27.
Kwa mujibu wa tovuti ya Soccer Base, msimu uliopita mechi yake ya
kwanza alicheza Septemba 13, 2015 dhidi ya Randers wakiwa ugenini,
ambapo walifungwa 1-0. Na ya pili msimu huo, walikuwa nyumbani dhidi ya
Hobro IK Novemba 29, 2015 walishinda mabao 2-0.
Msimu huu alicheza mechi ya kwanza Agosti 21, mwaka huu wakiwa
nyumbani dhidi ya Midtjylland walitoka sare ya mabao 2-2 na ule wa pili
alicheza Novemba 6, mwaka huu wakiwa ugenini dhidi ya FC Copenhagen,
ambapo walifungwa 4-0 na siku hiyo alipewa kadi ya kwanza ya njano.
Timu hiyo ina jumla ya wachezaji 45 lakini kati ya hao, kuna watano,
ambao hawajawahi kucheza kabisa. Pia, wachezaji wanaocheza kikosi
kikubwa wapo 27 kati ya hao 45 akiwemo yeye. Sio peke yake kucheza mechi
mbili tu msimu huu, kuna wengine wamecheza mechi moja tu, na wengine
hawajawahi kabisa.
Kutokana na kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha SonderjyskE,
klabu yake ya zamani ya Simba imeonesha nia ya kumrejesha akikumbukwa
kwa rekodi bora aliyoiweka misimu kadhaa iliyopita, ikiwemo kuisaidia
timu hiyo kutwaa ubingwa miaka kadhaa iliyopita.
Simba iko tayari kulipa dola za Marekani 120,000 ambazo ni sawa na Sh
milioni 240 kwa klabu hiyo ya Denmark kwa ajili ya kumrejesha Okwi.
Inaelezwa kuwa iwapo kiasi hicho cha fedha kitalipwa mchezaji huyo
atakuja kusaini mkataba wa mwaka mmoja kwa mshahara tu bila dau la
kumsainisha.
Simba iliwahi pia, kumuuza Okwi Etoile du Sahel ya Tunisia mwaka 2013
kwa dola 300,000 lakini hakudumu baada ya kuingia nao kwenye mgogoro na
kurudi kwao kucheza SC Villa ya Uganda mwaka huo, na baadaye kujiunga
na Yanga ambako alicheza muda mfupi na kurudi Simba.
CREDIT- GRACE MKONJERA/HABARI LEO
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: