
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
MAKAO Makuu ya Jeshi la Polisi nchini imesema inachunguza tuhuma
zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda dhidi ya
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi
Simon Sirro na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi
Suzan Kaganda kuhongwa ili wasidhibiti matumizi ya dawa za kulevya aina
ya shisha.
Makonda alitoa tuhuma hizo baada ya kudai kuwa viongozi hao wa polisi
wamekuwa wakilegalega kusimamia ipasavyo kukomesha matumizi ya dawa za
kulevya, aina ya shisha.
Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai katika makao makuu
ya jeshi hilo, Kamishna wa Polisi, Robert Boaz alisema hayo jana wakati
akijibu swali kuhusu hatua za jeshi hilo zilizochukuliwa kutokana na
tuhuma zilizotolewa na Makonda. “..kama ilivyo taratibu zetu tunapopokea
tuhuma dhidi ya kiongozi wa jeshi hili au askari yeyote tunafanya
uchunguzi, kwa hiyo hata tuhuma hizi tunazifanyia uchunguzi kubaini kama
ni kweli,” alisema alisema Boaz.
Wiki hii wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya
Umeme katika Jiji la Dar es Salaam uliofanywa na Waziri Mkuu, Makonda
aliwatuhumu viongozi hao wa polisi kwa kulegalega kusimamia suala hilo
huku akihofia wanaweza kuwa wamehongwa na watu waliotaka kumhonga yeye
lakini akakataa.
Lakini mkuu huyo wa mkoa alienda mbali zaidi na kudai kuna kikundi
cha watu 10 waliokwenda kwake ambao anawatambua kama “maajenti wa
shetani” ambao wanapata faida kati ya Sh milioni 35 mpaka Sh milioni 45
kwa mwezi kutokana na dawa hizo za kulevya.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: