HUKUMU ya mwanamume nchini Malawi aliyesema amefanya ngono na wasichana na wanawake takribani 104 kama sehemu ya kuwatoa nuksi huku akijua kwamba anaishi na virusi vya Ukimwi (VVU) inatarajiwa kutoka wakati wowote.


Mtu huyo alikamatwa baada ya kufanya mazungumzo ya kina na Shirika la Utangazaji la Uingereza kuhusu ufanyaji huo mapenzi wenye lengo la kuondoa nuksi kwa wanawake na pia kuwaingiza ukubwani mabinti.

Mwanamume huyo Eric Aniva alikamatwa nyumbani kwake Julai mwaka huu baada ya kukiri kwamba alifanya mapenzi na mabinti ambao wengine walikuwa ni watoto wa miaka 12 huku akijua kwamba anaishi na VVU.

Aidha, hali yake hiyo hakuwahi kumweleza mtu yeyote aliyekuwa anamtumia kama sehemu ya utamaduni wa eneo analotoka.

Aniva anasema kwamba alikuwa anakodishwa na ndugu wa mabinti hao kufanya nao ngono kama sehemu ya kuwaingiza ukubwani na wakubwa kuwaondoa nuksi hasa waliofiwa.

Inaaminika kwamba kama mwanamke aliyefiwa hatafanyiwa matendo hayo anaweza kuandamwa na bahati mbaya, kifo cha ghafla na hata ugonjwa.

Wakati Rais wa Malawi, Peter Mutharika alipotoa agizo la Aniva akamatwe na ashitakiwe kwa kubaka hakuna msichana aliyejitokeza kutoa ushahidi dhidi yake.

Kutokana na mazingira hayo, alibadilishiwa mashtaka na kushtakiwa kwa kujihusisha na utamaduni ambao ni hatarishi kwa mujibu wa kifungu cha tano cha sheria ya usawa wa jinsia ambapo alituhumiwa kufanya mapenzi na wajane.

Katika shitaka hili wanawake wawili wamejitokeza kutoa ushahidi dhidi ya Aniva ambapo mmoja alisema alifanyiwa kitendo hicho kabla ya matendo hayo kupigwa marufuku huku mwingine akisema alifanikiwa kutoroka kabla ya kuingiliwa kimwili.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: