KOCHA Hans Pluijm amesema wakati wowote atakabidhi taarifa ya benchi la ufundi kwa ajili ya kuanza kufanyiwa kazi na Kocha mpya George Lwandamina anayetarajiwa kuanza kazi mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.


Akizungumza , Pluijm alisema taarifa yake haijakamilika lakini anaendelea kuiandaa na wakati wowote ataikabidhi.

“Nimeanza kuiandaa taarifa, wakati wowote nitakabidhi,”alisema Pluijm huku akisema suala hilo aachiwe yeye na uongozi wa Yanga.

Lwandamina amenukuliwa kwenye vyombo vya habari kuwa anasubiri taarifa hiyo kuanza kazi mara moja. Lwandamina alisema anaijua Yanga kupitia DVD alizotazama na huenda akabadilisha kikosi na pengine mfumo.

Hata hivyo, bado uongozi wa Yanga haujatoa taarifa rasmi kuhusu hatma ya Kocha Hans Pluijm ingawa kunaelezwa kuna mazungumzo ya kumshawishi Pluijm kuwa Mkurugenzi wa benchi la ufundi, na nafasi ya Kocha iwe ya Lwandamina.

Kocha huyo Mholanzi alisema ni kweli anaendelea na mazungumzo na Yanga ili kujua hatma yake.

Pluijm hakutaka kuweka wazi juu ya kinachoendelea, ambapo alisisitiza kuwa uongozi wa Yanga ndio wenye nafasi ya kuzungumzia yale yanayoendelea kati yao.

Kocha huyo hivi karibuni aliandika barua ya kujiuzulu baada ya Yanga kufanya mazungumzo ya kumchukua kocha Mzambia bila ya kumhusisha Mholanzi huyo, ambaye aliahidiwa kupewa ukurugenzi wa ufundi.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ndiye aliyemshawishi kufuta uamuzi wake wa awali wa kujiuzulu nafasi hiyo.
 
DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: