Wawakilishi wa Tanzania katika tuzo za wanamuziki bora zinazoandaliwa na MTV Africa Music Awards 2016 (MAMA)  hawakufanikiwa kutwaa tuzo yoyote japokuwa waliweza kushiriki katika vipengele tofauti.


Katika tuzo hizo zilizotolewa Johannesburg, Afrika Kusini kuamkia leo, dalili zilionekana mapema kuwa mbaya kwani Vanessa Mdee aliyekuwa anawania tuzo ya msanii bora wa kike alishindwa baada ya Yemi Alade (Nigeria) kutangazwa mshindi.

Kama hiyo haitoshi, Diamond Platinumz aliyekuwa anashindania tuzo ya msanii bora wa mwaka akipambana vikali na Black Coffee, Sauti Sol, Wizkid na Yemi Alade alishuhudia tuzo hiyo akikabidhiwa Wizkid.

Wimbo “Unconditionally Bae” ulioimbwa na Sauti Sol akishirikiana na Alikiba, ambao ulikuwa kwenye kipengele cha wimbo bora wa kushirikishwa haukupata tuzo. Wimbo huo pia uliambulia patupu katika kipengele cha wimbo bora wa mwaka.

Hata hivyo, Yamoto Band iliyoshiriki katika tuzo hizo katika kipengele cha ‘Chaguo la Wasilikizaji’ haikufanikiwa kutwaa tuzo hiyo.

Msanii mwingine kutoka Tanzania aliyeshiriki tuzo hizo maarufu barani Afrika na kushindwa kufurukuta katika medani hiyo ya kimataifa ni Raymond.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: