
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Jeuri ya fedha, hicho ndicho unachoweza kusema kwa Serena Williams aliyevaa gauni la harusi βsheraβ lenye thamani ya pauni 2.6milioni (zaidi ya Sh Bilioni 5) katika harusi yake na mchumba wake Alexis Ohanian.
Serena na mumewe Ohanian walitoa picha zao za kwanza za harusi yao iliyoghalimu dola 1milioni iliyofungwa Alhamisi.
Nyota huyo wa tenisi (36), alipendeza na gauni ya thamani pauni 2.6milioni iliyotegenezwa na Sarah Burton kwa mtindo wa Alexander McQueen, gauni hilo kubwa limelembwa kwa dhahabu XIV Karats jewellery. Wakati bwana harusi Alexis (34) alikuwa amevaa koti na suruali ya kijivu kutoka kwa Armani.
Ohanian aliandika katika picha yake: "Wewe ni mwanamke bora wa wakati wote, siyo tu katika michezo, ila nazungumzia kuhusu mama na mke wangu."
Katika harusi hiyo wageni wote walipewa zawadi kikombe cha kipekee cha dhahabu kutoka kwa bi harusi Williams. Meza zote za wageni zilipewa majina ya mataji 12 grand slam aliyoshinda Williams.
Wawili hao wamekuwa pamoja tangu 2015 na ndoa yao inakuja wiki 11 tu tangu walipopata mtoto wao wa kwanza, binti Alexis Olympia Ohanian Jr aliyezaliwa Septemba Mosi. Alexis ni mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Reddit.
Watu maarufu waliohudhuria harusi hiyo ni pamoja na Beyonce, Kim Kardashian, Caroline Wozniacki na Eva Longoria. Kim aliwasili kwa ndege ya kukodi akiwa na rafiki wa dada yake, Khloe, Malika Haqq na dada yake Malika, Khadija. Mrembo Caroline Wozniaci yeye aliambatana na mchumba wake mpya, staa wa NBA, David Lee.
Dada wa Serena, Venus alipiga kivazi matata kabisa, huku mama yao Oracene Price, aliyekuwa amepiga kigauni kifupi cha zambarau pamoja na koti refu kwa nje.
Post A Comment: