WAATHIRIKA wa Ukimwi wanakabiliwa na hatari ya kuugua magonjwa yasiyoambukiza ya saratani na kupata matatizo ya misuli ya moyo, kutokana na athari za matumizi ya Dawa za Kupunguza Makali ya Virusi vya Ukimwi (ARV).

Utafiti mpya uliochapishwa juzi na Taasisi Utafiti wa Saratani na Virusi Vinavyosababisha Ukimwi (VVU) ya Chuo Kikuu cha Califonia, San Francisco (UCSF), umeeleza kuwa saratani hutokea katika tishu za mwili, ambako virusi hivyo hukimbilia kujificha ili visifikiwe na ARV.

Taarifa ya Mtaalamu wa Maabara, Profesa Michael McGrath wa  UCSF iliyochapishwa katika jarida la Virology la mwezi huu, imeeleza     imependekeza utafiti wa haraka ufanyike ili kutafuta muafaka wa tatizo hilo.

Wanasayansi hao wameelezwa kuwa walifanya utafiti huo baada ya kubaini kuwa baadhi ya waathirika wa VVU wanaotumia ARV na kuwa na afya nzuri, hujikuta wakifa ghafla.

“Baada ya kuchunguza tukabaini kuwa vifo hivi vinasababishwa na saratani pamoja na matatizo ya misuli ya moyo,” alisema Profesa McGrath.

Hali hiyo, anasema iliwafanya waendelee na utafiti ambao matokeo yake wameyapata mwezi huu kwa kubaini kuwa virusi vinavyojiviche kwenye tishu za mwili ambako havifikiwi na ARV ndivyo vinasababisha tatizo hilo.

Tangu dawa za ARV zianze kutumika zimeonekana kuzuia VVU kuathiri seli nyeupe za binadamu maarufu kama CD4.

Matumizi hayo yameweza kuwafanya baadhi ya waathirika kupima na kutoonekana tena kuwa na VVU kwenye mfumo wao wa damu lakini wakiacha kutumia ARV huzuka ghafla na kuanza kuonekana vikishambulia CD4.

Profesa McGrath anasema kuwa katika utafiti wao wamebaini kuwa kwenye tishu za mwili wa binadamu ambako VVU hujificha vinasababisha tatizo la saratani na matatizo ya moyo.

“Hivi vifo vya wagonjwa walio katika matumizi ya ARV vinaelekea vinatokana na uwapo wa virusi hawa waliojificha kwenye tishu baada ya kushindikana kufikiwa na dawa ya kuwaangamiza,” alisema Profesa McGrath na akifafanua:
 
DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: