NYOTA wa muziki nchini Nigeria waliokuwa wanaunda Kundi la P-Square, Peter na Paul Okoye, wametangaza kuuza nyumba yao iliyopo jijini Lagos.


Hatua hiyo imefikia mara baada ya kundi hilo kuvunjika kutokana na migogoro na kifamilia, huku Peter akidai kaka yao Jude Okoye alimtishia maisha na mke wake, hivyo hawawezi kuwa karibu tena hata kama ni familia moja.

β€œNaomba niweke wazi kuwa P-Square haipo tena na haiwezekani, kila mmoja anafanya yake sasa hata kama Paul anaandika kwenye kurasa zake za Instagram kwamba damu ni mzito kuliko maji, sasa nani damu na nani maji?

β€œKila mtu anatakiwa kuishi na mambo yake, ndiyo maana ni bora kuuuza nyumba yetu, kila mtu afe na chake,” alisema Peter.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: