Kama bado unaamini kuwa Hamisa Mobeto anamtumia mtoto wake kujiweka karibu na Diamond, ujumbe huu unakuhusu.


Hamisa amewashangaa watu wanaodai kuwa anamtumia mtoto wake na kudai kuwa hana sababu ya kufanya hivyo.

Mrembo huyo amesema kuwa hakuna kipya anachokiona kwa Diamond kwa sasa kwani amekuwa naye kwa miaka tisa.

 "Sioni kipya wala cha ajabu mtu nimeshakuwa naye kwa miaka tisa, iweje leo niambiwe namtumia mtoto,"

 Kuhusu utata wa jina la mtoto wake Hamisa amesema akiwa na ujauzito yeye na Diamond walikubaliana wamuite mtoto huyo Abdul Latif.

 "Alitaka aitwe hivyo ili lifanane na mwane Latifa, lakini baadaye akasema aitwe Daylan ili liendane na Nillan.

 "Kuna wakati alikataa ujauzito hadharani nami nikaamua mwanangu aitwe Abdulnaseeb ila kwa sasa nimekubali anaitwa Dylan Abdul Naseeb," amesema

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: