
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
MKUU wa Wilaya ya Malinyi mkoa wa Morogoro, Majura Kasika ameagiza
posho iliyookolewa kutokana na kufutwa kwa safari ya maofisa watatu na
madereva wawili wa wilaya hiyo kwenda kwenye kilele cha mbio za Mwenge
wa Uhuru kitaifa mwaka huu mkoani Simiyu, kuelekezwa katika kuongezea
nguvu ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu sita ya vyoo.
Hatua ya viongozi hao kufuta safari hiyo, ilitokana na agizo la Rais
John Magufuli aliyeagiza viongozi kutoka mikoa yote nchini, nje ya
Simiyu, kutokwenda katika maadhimisho hayo na wale ambao walikuwa tayari
wamechukua posho kuzirejesha mara moja.
Kasika alisema jana kuwa kutokana na agizo hilo la Rais, wilaya ya
Ulanga iliweza kuokoa Sh 2, 580,000 ambazo sasa zitaelekezwa katika
kuchangia ujenzi huo wa vyumba viwili vya madarasa na matundu ya vyoo
katika Shule ya Msingi ya Kitongoji cha Lumbanga Kijiji cha Misegesege
Kata ya Malinyi.
Akizungumza na wananchi wa kitongoji hicho cha Lumbanga, wakati
akiendesha kazi ya uhamasishaji wa uchangiaji wa michango ya maendeleo
kwa ajili ya kupata fedha za kuanza kufyatua matofali ya ujenzi huo,
Mkuu huyo wa wilaya alisema fedha hizo zitaelekezwa mara moja katika
mradi huo.
Uamuzi huo wa Mkuu wa Wilaya, uliungwa mkono na Mbunge wa Malinyi, Dk
Haji Mponda ambaye aliahidi kuchangia Sh 500,000 katika mpango huo,
huku wananchi wakiahidi kuchangia Sh 30,000 kwa kila kaya.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: