Serikali imepiga marufuku viwanda kuzalisha mifuko ya platiki kuanzia Januari mwakani.


Akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira mjini hapa jana, Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira, Richard Muyungi amesema wanachosema wabunge hakina tofauti na kilichoandikwa kwenye kanuni zinazoandaliwa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa uamuzi huo.

β€œSisi katika kanuni zetu tumewapa miaka miwili ya kubadilisha teknolojia hiyo kwenda katika uzalishaji wa mifuko inayooza ili kuepuka athari za mazingira,” amesema Muyungi.

Amesema mwaka 2013 walisitisha kusajili viwanda vya kuzalisha mifuko ya plastiki ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

Kuhusu viwanda vyenye malighafi ya kutengenezea mifuko hiyo, mwanasheria katika ofisi hiyo, Isakwisa Mwamukonda amesema kanuni hizo zinawapa nafasi wawekezaji kuzalisha mifuko hiyo hadi zitakapomalizika, lakini hawataruhusiwa kuiuza hapa nchini.
DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: