NI kama mauzauza ya kijana, Isack Ernest, aliyepigwa akishukiwa kuwa mwizi kiasi cha kudhaniwa amekufa na kupelekwa mochari ya Hospitali ya Temeke.

Wakati kijana huyo akisimulia mkasa uliomkuta mwanzoni mwa wiki iliyopita, jana baba yake aliieleza  alivyopata taarifa hizo zilizozua taharuki katika familia yake.

Hata hivyo, wakati baba huyo, Ernest Chalo akieleza mkasa mzima ikiwa ni pamoja na msimamizi wa mochari kumvua nguo maiti mwingine na kumvisha Isack anayedaiwa kuzinduka chumbani humo, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Agustino Mosha alisema katika hospitali hiyo hapakuwa na maiti aliyezinduka mochari.

Kwa upande mwingine Jeshi la Polisi nalo likigoma kueleza Isack alivyokuwa alipopokewa, kwa madai kuwa ni kazi ya madaktari.

Jumamosi iliyopita, kijana huyo wa kidato cha tatu wa  sekondari ya Lumo alipigwa na wananchi akidaiwa kuhusika na tukio la uporaji wakati akirejea nyumbani baada ya kuangalia tamasha la muziki wa Singeli, Mbagala Zakheim. Katika tukio hilo, kijana Seleman Hamisi aliuawa.

Dk Mosha alisema siku ya tukio walipokea maiti wawili, Selemani Selenge (16) ambaye mwili wake utasafirishwa kwenda Musoma na Kelvin Ally (14) ambaye mwili wake ulichukuliwa Oktoba 17.

Alibainisha kuwa hakuna kijana aliyefikishwa mochari na kuzinduka.

“Katika hospitali kuna utaratibu wa kupima maiti; mapigo ya moyo na mboni za macho ili kujua kama mtu amekufa au la. Ni kinyume cha sheria kuhifadhi mochari mtu hai,” alisema.

"Navisihi vyombo vya habari visitoe taarifa za uongo kwa jamii wakati havijazifanyia kazi kujua ukweli wake,” alisema daktari huyo katika mahojiano.

Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Temeke, Gilles Murato alipoulizwa kuhusu habari hizo, alisema hawezi kuzungumzia masuala ya hospitali.

Baba

Akizungumzia tukio hilo, Chalo alisema akiwa nyumbani alipigiwa simu na mtu asiyemfahamu akimtaka aende hospitali ya Temeke na nguo za kumvisha mwanawe ambaye alizinduka akiwa mochari baada ya kufikishwa hapo na Polisi.

“Baada ya taarifa hiyo nilishituka kwa kweli. Nilimtafuta Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na baada ya kufika hatukuona mwili zaidi ya kushuhudia gari la Polisi likiondoka,” alisema.

"Nilipokwenda mochari, nilikuta mtu mmoja na kunieleza kuwa yeye ndiye msimamizi wa chumba hicho na kwamba mwanangu alizinduka hivyo yeye akamvua nguo maiti mwingine ili kumsitiri (Isack).”

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  





ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: