KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeibana Wizara ya Fedha na Mipango juu ya kutumia zaidi ya Sh. bilioni 48 zilizotengwa kusaidia wafanyabiashara walioathirika na mdororo wa uchumi uliotokea mwaka 2007/8.


Wizara hiyo ilitoa fedha hizo ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kuwainua wafanyabiashara walioathiriwa na hali hiyo, lakini hadi sasa bado haijulikani ni kampuni zipi zilipewa na shughuli zilizofanyika.

Katika kikao chake cha jana kilichofanyika bungeni mjini hapa, kamati hiyo wakati ikipitia ukaguzi fungu namba 21 linalohusu Hazina, ilimbana Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo upande wa huduma za fedha, Doroth Mwanyika na kumtaka kueleza fedha hizo zilikokwenda.

Mbunge wa Vwawa (CCM), Japhet Hasunga, alisema mwaka huo kulikuwa na mdororo mkubwa wa uchumi na nchi zingine zilichukua hatua mbalimbali za kupambana na hali hiyo na Tanzania iliamua kupambana kwa kutumia zaidi ya Sh. bilioni 48 kukuza uchumi.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: