MTU  anayepata fursa ya kufika nchini Senegal, Afrika Magharibi,  ni vyema pia akakitembelea kisiwa cha Gorée kilichopo kilomita tatu kutoka pwani ya Jiji la Dakar ambapo, miongoni mwa mambo mengine, ataona  kile kiitwacho kwa Kiingereza ‘Door of No Return’ yaani mlango ambao ukishaupita hutaweza kurejea tena.


Mlango huo upo katika jengo kubwa la zamani lijulikanano kama ‘House of Slaves’ au Jumba la Watumwa.  Kwa Kifaransa linaitwa ‘Maison des Esclaves’.  Mlango huo ulikuwa ndiyo mapito ya mwisho ya Waafrika waliokuwa wanasombwa kwa mamilioni kwenda utumwani sehemu mbalimbali duniani, hususani Bara la Amerika. 
Rais Barack Obama na mkewe wakiwa ‘Door of No Return’  walipotembelea kisiwa cha Gorée Juni 27, 2013.

Kwa mtumwa ukiupita mlango huo basi unaelekea moja kwa moja kwenye majahazi au meli zilizokuwa zimetia nanga na kuanza safari ya maelfu ya maili kwenda utumwani ambako walilowea  kwenda kufanyishwa kazi kwa nguvu, wakafia huo na kuacha vizazi ambavyo hadi leo vipo Marekani, Uingereza, Cuba na kadhalika.

Jengo hilo lililokarabatiwa kidogo, lilijengwa mnamo 1776 na kuendelea kuweka namba kubwa ya watumwa hadi mwanzoni mwa miaka ya 1800, pamoja na takwimu zinazokinzana hasa kutoka kwa Wazungu, mlango wake unaaminika ulipitisha Waafrika zaidi ya milioni 15 kwenda utumwani hususan Amerika.
Obama akiangalia mandhari ya eneo hilo.

Jumba hilo pamoja na kuwa kivutio cha kusikitisha kwa Waafrika, limetembelewa na watu kibao duniani wakiwemo Papa John Paul wa Pili, Rais Barack Obama, na marehemu Nelson Mandela ambaye kufika kwake hapo kulimtoa machozi hadharani.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: