
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
VIWANDA 22 vinatarajiwa kujengwa nchini na Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii, ikiwa ni utekelezaji wa mwito wa Serikali wa kuzitaka hifadhi ya
jamii kuwekeza na kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini.
Katika utekelezaji wa agizo hilo, mifuko ambayo imeshaanza
utekelezaji ni NSSF, PPF, PSFP, LAPF, GEPF wakati Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF) nao tayari umeanza kufanya mapitio ya kina kwa ajili ya
kuwekeza katika uzalishaji maeneo mbalimbali, yenye lengo la kuimarisha
upatikanaji wa dawa hospitalini.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (TSSA),
Meshack Bandawe alisema jana mjini hapa kuwa hatua hiyo ya mifuko ya
hifadhi ya jamii ya kujikita katika uwekezaji wa viwanda, itasaidia
asilimia 40 ya ongezeko la ajira nchini itokane na sekta ya viwanda.
Alikuwa akizungumza katika mkutano wa sita wa wadau wa mfuko wa NSSF, unaofanyika mjini hapa.
Katika uwekezaji huo, PPF imeanza mchakato wa ujenzi wa jengo la
uzalishaji kwa ajili ya kampuni ya nguo ya TOOKU na kiwanda hicho
kinajengwa katika eneo huru la kiuchumi la Benjamin Mkapa jijini Dar es
Salaam.
Mfuko huo pia utapanua kiwanda cha viatu cha magereza kilichoko
Karanga mkoani Kilimanjaro kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza na pia
watafanya kwa ubia na NSSF katika kujenga kiwanda cha sukari huko
Mkulazi mkoani Morogoro.
Bandawe alisema mfuko wa PSPF utajenga eneo maalumu la kiuchumi
katika eneo la Kurasini, ambako kitakuwa ni kituo cha bidhaa zinazotoka
China na itajenga kiwanda cha kutengeneza Agave Syrup kutokana na mabaki
ya mkonge mkoani Tanga.
Mfuko wa LAPF utafufua Kiwanda cha Chai cha Mponde kilichoko Lushoto,
Tanga na watajenga kiwanda cha kutengeneza bidhaa za hospitali na
majitiba. Kwa upande wa Mfuko wa GEPF utafanya mradi wa ujenzi na
ufufuaji wa kiwanda cha kuchonga vipuri katika eneo la Kilimanjaro
Machine Tools mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Mfuko huo pia utajenga machinjio ya kisasa kwa kushirikiana na
Kampuni ya Ranchi za Taifa (Narco) na Benki ya Uwekezaji (TIB) huko
Tandahimba, Mtwara na kujenga kiwanda cha kusindika juisi na mvinyo
utokanao na zabibu huko Chinangali mkoani Dodoma na watafufua na
kuendeleza kiwanda cha kubangua korosho cha Tandahimba mkoani Mtwara.
Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (TSSA) wao wamejipanga
kufufua na kuendeleza uanzishwaji viwanda vipya vya sekta ya nguo na
mavazi, ufufuaji na uendelezaji wa viwanda vipya vya sekta ya ngozi na
bidhaa za ngozi na uanzishwaji wa viwanda vipya vya uchongaji wa vipuri.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara alisema mfuko wake
umedhamiria kuwekeza zaidi kwenye viwanda vya kusindika nafaka pamoja na
mafuta ya kula.
Aliongeza kuwa uwekezaji katika maeneo hayo, hauhitaji mitaji
mikubwa. Alisema kiwanda cha sukari ambacho wanakijenga kwa ubia na PPF,
kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 200,000 kwa mwaka na kitatoa ajira
kwa watu wapatao 100,000.
Profesa Kahyarara alisema NSSF imejipanga kufufua vinu vya usagaji wa
nafaka vya NMC vilivyopo Iringa, Dodoma na Arusha, watafufua kiwanda
cha matairi cha Arusha (General Tyre) na pia wanakamilisha uzalishaji wa
majaribio wa kiwanda cha viuadudu kilichoko Kibaha, mkoani Pwani.
Mfuko wa NHIF kwa kuanzia unatafanya mradi wa uzalishaji dawa na
bidhaa hospitalini, uzalishaji wa maji tiba na uzalishaji wa gesi kwa
ajili ya tiba. Kutokana na kujikita katika maeneo hayo, mfuko huo
umepanga kufufua viwanda vilivyopo katika hospitali mbalimbali kwa ajili
ya utengenezaji wa maji tiba.
Pia watajenga kiwanda cha uzalishaji wa bidhaa za hospitali kwa ubia
na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, watajenga kiwanda cha uzalishaji
dawa kali kwa ubia na Bohari Kuu ya Dawa (MSD), watajenga kiwanda cha
uzalishaji wa gesi ya oksijeni katika Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili
(MOI).
Bandawe alisema mfuko huo, pia utafanya uwekezaji kwa kushirikiana na
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika kufufua uzalishaji wa dawa katika
kiwanda cha dawa kinachomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa cha Mgulani;
na kujenga kiwanda kipya kikubwa cha kisasa kwa ajili ya kuzalisha dawa
pamoja na bidhaa mbalimbali za hospitali katika kambi ya Ruvu.
Alisema mfuko wa ZSSF umejipanga kuingia katika uvuvi wa bahari kuu
na usindikaji wa samaki na kuongeza kuwa mfuko huo uko tayari kushiriki
katika miradi ya pamoja itakayotekelezwa na TSSA.
“Miradi yote hii tunashirikiana na Benki ya Azania ambayo mifuko yote
ni wabia na tunataka kuifanya benki hii iwe ya viwanda. Pia
tutashirikiana na JKT katika utekelezaji wa miradi hiyo,” alisema
Bandawe.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: