
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
SIKU chache baada ya mrembo wa Bongo Movies, Wema Sepetu kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM), imebainika yapo mambo matatu yaliyomsababisha mrembo huyo arejee na kuachana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Kabla ya kufanya uamuzi huo Ijumaa iliyopita, Wema na mama yake mzazi, Miriam Sepetu, waliokuwa makada wa CCM, Februari 24, mwaka huu, walitangaza kujiunga na Chadema wakidai wanaifuata demokrasia ya kweli.
Hata hivyo, mama wa mrembo huyo, aliitisha mkutano wa waandishi wa habari na kusema yeye hana mpango wa kurejea tena CCM na atamalizia maisha yake duniani akiwa Chadema.
Chanzo kilicho karibu na Wema, kimeeleza kuwa, mambo ambayo yamemfanya mrembo huyo arudi CCM ni pamoja na lile alilolianisha mwenyewe wakati alipotangaza kurejea chama hicho tawala.
βJambo la kwanza kabisa ni amani ya moyo. Kama ulivyosikia siku ile alipotangaza kurudi CCM alisema kabisa hana sababu ya kubaki kwenye chama ambacho hakimpi amani ya moyo. Amerejea CCM ambako alikuwa anaipata,β kilisema chanzo hicho.
Ukiachana na hilo, chanzo hicho kiliweka bayana kuwa, jambo lingine lililomsababisha mrembo huyo arejee CCM ni kitendo cha kuwaona viongozi mbalimbali wakubwa wakijiunga au kurejea CCM.
βWema aliamini kwamba viongozi aliowakuta, kina Lawrence Masha na wengineo wangeendelea kushikamana na kujenga chama lakini matokeo yake wimbi la wanaharakati wengi wa Chadema kukikimbia chama hicho limeongezeka,β kilisema chanzo hicho.
Aidha, chanzo hicho kililitaja jambo lingine lililosababisha Wema arejee katika chama hicho tawala ni pamoja na kutokabidhiwa kadi ya Chadema kwa muda mrefu.
βUnajua aliona kama anakosa zile confidence za kujinasibu kama ni Chadema damu. Hilo limemfanya aone kuna urahisi tu yeye kutoka kwani anakokupigania wala hakujamfunga kivile,β kilisema chanzo hicho.
Pamoja na hayo matatu, vyanzo vingine vimeeleza kuwa mrembo huyo amerejea CCM kwani kuna fursa za kazi mbalimbali ambazo anaweza kunufaika nazo tofauti na akiwa nje ya chama hicho.
Taarifa nyingine kutoka ndani ya familia zimeeleza pia, huenda baadaye mama wa mwingizaji huyo pia akamfuata mwanaye licha ya mwenyewe kukaririwa akisema kuwa hana mpango huo.
Post A Comment: