
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Chama cha Wananchi (CUF) upande unaomuunga mkono Mwenyekiti wa Taifa anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba umesimamisha wagombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa majimbo matatu.
Uchaguzi uliopangwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kufanyika Januari 13,2018 utafanyika katika majimbo ya Longido, Singida Kaskazini na Songea Mjini.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya amewataja wagombea hao na majimbo yao kwenye mabano kuwa ni Delfina Mlelwa (Singida Kaskazini), Japhary Mneke (Songea Mjini) na Kisiongo Mayasek Olukuya (Longido).
Uteuzi huo umefanyika siku chache baada ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutishia kutoshiriki uchaguzi huo endapo NEC haitasitisha mchakato na kujadili dosari zilizojitokeza katika uchaguzi wa awali.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwa niaba ya Ukawa, alisema uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata 43 uliofanyika Novemba 26,2017 ulikuwa na dosari zinazopaswa kujadiliwa kabla ya kufanyika uchaguzi mwingine.
Post A Comment: