
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kina uhakika wa kushinda uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Singida Kaskazini ambalo Bunge lilitangaza jana kuwa liko wazi.
Kutangazwa kuwa wazi kwa jimbo hilo, sasa kunatoa fursa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza mchakato wa kupata mrithi wa Lazaro Nyalandu ambaye alitangaza kujizulu nafasi hiyo na kujitoa uanachama wa CCM mwanzoni mwa wiki.
Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene, alipoulizwa kuhusu uchaguzi huo, alisema watamtangaza mgombea wake, baada ya Nec kutangaza kuhusu uchaguzi huo.
"Tutamtangaza mgombea wetu ambaye tutamsimamisha kwenye uchaguzi huo mdogo na tunaamini tutakayemsimamisha atashinda," alisema Makene.
Nipashe ilimtafuta Mkurugenzi wa NEC, Ramadhan Kailima, ili kujua kama tayari imeshapokea barua ya bunge na ni lini itatanganza uchaguzi mdogo, alisema muda ukifika watajulisha.
Jumatatu ya wiki hii, Nyalandu alitangaza kujiuzulu nafasi ya Ubunge na kutangaza kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Pia alisema amejiuzulu nafasi yake ya ujumbe wa Halmashauri Kuu CCM pamoja na nafasi zote za uongozi ndani ya chama tawala kuanzia siku hiyo.
Nyalandu alisema tayari alikuwa amemwandikia barua Spika Ndugai ya kujiuzulu ubunge alioutumikia kwa kipindi cha vipindi vinne mfululizo tangu alipochaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2000.
Aidha alitaja sababu za kuchukua uamuzi huo kuwa ni kutoridhishwa na mwenendo wa hali ya kisiasa nchini ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa haki za kibinadamu na ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania.
Kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya mihimili ya dola (Serikali, Bunge na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa kibunge wa kutunga sheria na wa kuisimamia serikali kutokuwa na uhuru ilioanishwa na kuwekwa bayana kikatiba, ilikuwa sababu nyingine iliyoelezwa na Nyalandu.
Pia alieleza kuwa, bila Tanzania kupata Katiba Mpya sasa, hakuna namna yeyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali, Bunge na mahakama ambayo ndio chimbuko la uongozi bora wa nchi, na kuonesha kwa uwazi kuwa madaraka yote yatokana na wananchi wenyewe, na kwamba serikali ni ya watu kwa ajili ya watu.
Post A Comment: