Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Hamphrey Polepole amesema kuwa chama hicho hakina taarifa yoyote ya kurudi kwa Wema Sepetu.


Akijibu swali kuhusu taarifa kuwa Wema amerudi CCM akitokea Chadema, Polepole amesema CCM ina utaratibu wa mwanachama kujiunga na chama hicho.

"Kupitia utaratibu na muundo wetu wa chama kwenye shina kisha ataandikwa kwenye orodha ya wanachama kwenye tawi ambalo yeye ni mkaazi," amesema

Hapo jana Wema Sepetu alitangaza kurudi CCM baada ya kukaa Chadema kwa muda wa miezi kumi tangu alipohamia.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Wema aliandika hivi, β€œSiwezi kuendelea kuishi kwenye nyumba inayonikosesha amani... Peace of mind is everything for me...natangaza rasmi kuondoka Chadema na kurudi nyumbani.”

Mwigizaji wa filamu ambaye pia ni kada wa CCM, Steve Nyerere alipoulizwa kuhusu msanii mwenzake huyo kurudi CCM alisema ni kweli amefanya hivyo.

Akizungumza na waandishi akiwa ameambatana na mama yake mzazi nyumbani kwao Sinza Jijini Dar es Salaam wakati akihamia Chadema, Wema alisema sababu kubwa ya kuhamia ni ili kupata nafasi ya kupigania demokrasia anayodai kuwa inapotea nchini Tanzania.

Sababu nyingine aliyoieleza Wema ni kutelekezwa na CCM licha ya kujitolea kutoa mchango wake kwa chama hicho wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 kiasi cha kuwa hatarini kumwagiwa tindikali visiwani Zanzibar.

Hata hivyo, jana alibadili msimamo wake na kurudi CCM. Akizungumzia kuhama kwa Wema, Meya wa Ubungo, Boniface Jacob ambaye alipokea kadi ya CCM kutoka kwa Wema, alisema walikuwa bado hawajamkabidhi msanii huyo kadi ya Chadema na kuwa walikuwa wanatafuta siku maalum ya kufanya hivyo.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: