MABINGWA wa soka Tanzania, Yanga leo ina kibarua kigumu mbele ya wenyeji wao Singida United kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Namfua.


Wakati wachezaji wa Yanga wakijiandaa na mchezo huo wa leo, kocha wa timu hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Sportpesa, George Lwandamina, amesema kuwa mchezo huo hautakuwa mwepesi.

Akizungumza na gazeti la Nipashe kutoka Singida, Lwandamina, alisema kuwa amekiandaa kikosi chake kupata ushindi huku pia akisisitiza kupata bao la mapema ili kuwachanganya wapinzani wao.

“Wao (Singida United) wapo nyumbani na watapata sapoti kubwa ya mashabiki wao…, litakuwa jambo zuri na lenye faida kwetu kama tutapata bao la mapema,” alisema Lwandamina.

Alisema ana imani kubwa na kikosi chake lakini watacheza kwa tahadhari dhidi ya wapinzani wao hao.

Wakati Lwandamina akisema hivyo, kocha wa Singida United ambao pia ni miongoni mwa timu zinazodhaminiwa na Sportpesa, Hans van de Pluijm, alisema Yanga wasitegemee mteremko kwenye mchezo huo.

Alisema anafahamu Yanga ni timu kubwa na yenye wachezaji bora, lakini timu yake ina nafasi kubwa ya kuondoka na ushindi kwenye mchezo huo.

“Naifahamu Yanga, wanawachezaji wazuri, lakini na sisi tumejiandaa vizuri kwa mchezo huu, kama nilivyosema hautakuwa mchezo
mwepesi kwao,” alisema Pluijm ambaye ni kocha wa zamani wa Yanga.

Ushindi kwa Yanga kwenye mchezo wa leo utawafanya kukaa kileleni angalau kwa masaa 24 kabla ya mchezo wa kesho kati ya Simba dhidi ya Mbeya City.

Simba wanaongoza ligi kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa ikiwa na pointi 16 sawa na Yanga, Azam FC na Mtibwa Sugar.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: