ads

Aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni (CUF), Maulid Mtulia amekabidhiwa kadi ya uanachama ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika ofisi za chama hicho tawi la Kondoni.


 Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi, Mtulia amesema amejivua nyadhifa zake zote alizokuwa nazo katika chama cha CUF ikiwamo Ubunge wa Jimbo la Kinondoni, na kuamua kujiunga na CCM kutokana na kuridhiswa na utendaji wa Rais Dk. John Magufuli."Mimi ni mgeni na salamu ninayoijua ya CCM ni CCM Oyeee" - Mtulia

"Nimejiunga na CCM ili kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na Rais Dk. Magufuli, Nimetoka kwenye chama chenye migogoro mingi, nimekuja kwenye chama chenye amani, haki na Demokrasia ya kweli, Ningekuwa Mbunge kupitia CCM ningefanya mengi makubwa zaidi, amesema Mtulia

Amesema hajafuata CCM cheo bali ametumia haki yake ya kidemokrasia ya kujiunga na chama chochote anachokitaka, na kwamba anawashangaa viongozi wa upinzani wanaopinga na kususa mambo ya serikali na shughuli za Bunge.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: