JARIDA mashuhuri la New African Magazine, limeanika orodha ya watu 100 mashuhuri zaidi Afrika kwa mwaka 2017. Watu hao ni kutoka katika mataifa 31 ya Afrika, wakiwemo marais watatu, wanawake 42 huku Wanigeria wakiongoza kwa kutoa watu 21 na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zikitoa watu 14 kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Rwanda na Uganda.


Kwa mujibu wa jarida hilo, kundi la Wanasiasa na Watumishi wa Umma waliong’ara kutoka Afrika Mashariki ni Jaji David Maraga wa Mahakama ya Juu ya Kenya, aliyejipatia umaarufu kutokana na `kutenda haki’ kwa kutengua matokeo ya urais wa Kenya katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo Agosti 8, mwaka huu.

Katika kundi hilo yumo pia Rais wa Rwanda, Paul Kagame akiwa ni Rais pekee wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika orodha hiyo. Pia wamo Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Amina Mohammed (Nigeria), Mwanasoka na mgombea urais wa Liberia, George Weah, Yemi Osinbajo –Makamu wa Rais (Nigeria), Rais wa Guinea Alpha Conde, Rais wa Ghana Nana Akufo- Addo, mwanasiasa wa Kenya, Sophia Abdi Noor na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI – King (Morocco).

Wengine katika kundi hilo ni Akinwumi Adesina, Rais wa Benki ya Maendelea Afrika (AfDB) (Nigeria), Vera Songwe, Mkuu wa Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa barani Afrika (Cameroon), Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika, Moussa Faki Mahamat (Chad).

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Dk Tedros Ghebreyesus (Ethiopia), mtaalamu wa lishe kutoka Kenya, Profesa Ruth Oniang’o, Waziri wa Fedha wa zamani wa Afrika Kusini, Pravin Gordan na Sibeth Ndiaye, raia wa Senegal ambaye ni Mshauri wa Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron.

Katika kundi la wafanyabiashara, bilionea namba moja Afrika, Aliko Dangote wa Nigeria ameingia kama ilivyo kwa bilionea kijana zaidi Afrika, Mohammed Dewji ambaye ni Mtanzania pekee katika orodha hiyo. Hata hivyo, Dewji ameungana na mfanyabiashara wa Kenya, James Mworia wa kampuni ambayo ndiyo pekee kutoka Afrika Mashariki
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: