Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amempongeza George Weah kwenye akaunti yake ya Twetter akiamini ameshinda uchaguzi Mkuu nchini Liberia huku matokeo rasmi yakiwa bado hayajatangazwa.


Wenger aliuvaa mkenge huo baada ya kusoma taarifa kwenye mtandao kuhusu ushindi wa uchaguzi wa Rais, nchini Liberia ambapo taarifa zinaeleza kwamba kazi ya kukamilisha matokeo ya mwisho bado inaendelea.

Kocha huyo aliandika, “Ninapenda kukupongeza mmoja wa wachezaji wa zamani ambaye umekuwa Rais wa Liberia, George Weah.

Hii sio mara ya kwanza kwa mchezaji wa zamani kuwa rais wa nchi na umefanya vyema George Weah…”

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: