Lazaro Samuel Nyalandu amekuwa mbunge wa kwanza katika Bunge la Kumi na Moja kujiondoa kutoka chama chake, ikiwa ni miaka miwili baada ya kuchaguliwa.


Jana mchana video za uamuzi wa kujiondoa CCM zilizagaa kwa kasi mitandaoni na baadaye Nyalandu, ambaye alikuwa mbunge wa Singida Kaskazini, kuithibitishia Mwananchi uamuzi huo wa kujivua nyadhifa zote kwenye chama.

Nyalandu, ambaye katika siku za karibuni alieleza nia ya kurejesha mchakato wa kuandika Katiba mpya kwa kuanzia Rasimu ya Warioba, ameeleza kuwa amechukua uamuzi huo kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa siasa nchini.

Uamuzi huo unamaanisha kuwa jimbo la Singida Kaskazini sasa litakuwa wazi mara baada ya Spika Job Ndugai kupokea barua ya Nyalandu na baadaye kuitaarifu Tume ya Uchaguzi (NEC), ambayo itaandaa uchaguzi mdogo.

Pamoja na kuwa mbunge wa kwanza kuachia ngazi katika Bunge la Sasa, Nyalandu si wa kwanza kufanya hivyo tangu siasa za ushindani zirejeshwe nchini. Augustine Mrema, aliyekuwa mbunge wa Moshi Vijijini, alijivua uanachama wa CCM mwaka 1995 baada ya kuvuliwa uwaziri kwa kosa la kutotunza siri za Baraza la Mawaziri. Mrema alijiunga na NCCR-Mageuzi na baadaye kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho.

Pia, Freddy Mpendazoe, aliyekuwa mbunge wa Kishapu, alijivua ubunge mwaka 2010 na kuasisi Chama cha Jamii (CCJ), wakati mfanyabiashara maarufu, Rostam Aziz alijivua uanachama wa CCM na kupumzika siasa wakati chama hicho kikiwa katika mkakati wa “kujivua gamba”.

Mwaka 2010, Zitto Kabwe, aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini, alijivua uanachama wa Chadema mwaka 2015 na baadaye kujiunga na ACT-Wazalendo.

Hata hivyo, mazingira ya kujiondoa kwake yanamfanya awe mbunge wa pili kuondoka kwenye chama chake bila ya kuwepo tishio la kutimuliwa, akimfuatia Mpendazoe. Zitto na Mrema walijiondoa vyama vyao kukiwa na uwezekano wa kutimuliwa. Zitto alijitoa mara baada ya kushindwa katika kesi yake kuizuia Kamati Kuu ya Chadema kumjadili na kutoa uamuzi dhidi yake, wakati Mrema alizungumzia bungeni suala la kashfa ya matumizi mabaya ya fedha za Debt Conversion Program yaliyofanywa na mfanyabiashara maarufu, P.V Chavda, suala ambalo lilishazungumziwa na Baraza la Mawaziri.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: