ads

BENKI ya Dunia (WB) imesifu Mahakama ya Tanzania kwa kasi nzuri inayoenda nayo katika utekelezaji wa Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama pamoja na Mpango Mkakati wa miaka mitano (2015/16-2019/2010) wa Mahakama.


Pongezi hizo zilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mtaalamu Mwandamizi wa Maboresho ya Utumishi wa Umma kutoka WB, Waleed Malik.

Malik alikuwa akizungumza katika kikao cha majumuisho na wajumbe wa menejimenti ya Mahakama ya Tanzania baada ya ziara ya ujumbe wa WB.

“Kufuatia ziara tuliyofanya ya kukagua na kujionea maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama, tumeona mnaendelea vizuri na ninapenda kuwapongeza kwa ushirikiano wenu," alisema Malik.

Malik alisema Mahakama ni moja kati ya taasisi zinazokwenda vizuri katika utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Benki ya Dunia nchini.

Mbali na pongezi, Malik aliisihi menejimenti ya Mahakama kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika kuwapa mafunzo ya matumizi ya TEHAMA watumishi wake ili maboresho yanayofanyika yatekelezeke vizuri.

“Ni muhimu kuwapa mafunzo ya TEHAMA watumishi wa kada mbalimbali wa Mahakama ili mifumo ya kielektroniki itakayowekwa iweze kutumiwa na watumishi bila shida yoyote,” alisema zaidi mtaalamu huyo kutoka Benki ya Dunia.

Alishauri pia juu ya umuhimu wa kuimarisha utoaji taarifa kwa jamii ili wananchi waweze kujua juu ya maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanyika ndani ya Mahakama ya Tanzania.

UTOAJI HAKIAkizungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mtendaji Mahakama ya Rufani, Sollanus Nyimbi aliahidi kufanyia kazi maelekezo na changamoto zilizoibuliwa na Benki ya Dunia ili kuendana na matakwa ya utekelezaji wa Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama.

“Tunashukuru kwa pongezi, lakini pia tunaahidi kufanyia kazi yale yote mliyoyaibua lengo likiwa ni kuboresha huduma ya utoaji haki nchini,” alisema Nyimbi.

Ujumbe huo wa WB uliwasili Desemba 4, lengo likiwa ni kukagua utekelezaji wa Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama pamoja na Mpango Mkakati wa miaka mitano (2015/16-2019/2010) wa Mahakama.

Ujumbe huo pia ulipata wasaa wa kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Mafunzo cha Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kilichojengwa eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mradi wa Ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Kawe pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Mahakama ya Wilaya Kigamboni.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: