ads

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. John Magufuli amemshukuru Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kwa kutoangalia rushwa wala urafiki pindi alipomchagua kugombea urais na kutaka wanachama wake kuchagua wajumbe wa Halmashauri Kuu wenye mapenzi ya dhati na chama.


 Dkt. Magufuli ameonya hayo wakati  akifungua mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma jana ambapo  amesema chama hicho kimedhamiria kupambana na rushwa na kwamba kama Rais Mstaafu Jakaya Kikwete angeangalia hayo basi yeye asingepata nafasi alonayo

“Msichague watu kwa urafiki au kwa sababu ya rushwa, binafsi napenda nimshukuru mzee Kikwete (Jakaya) yeye hakuangalia rushwa nadhani angefanya hivyo huenda mimi nisingepita,” amesema.

Aidha Dkt. Magufuli amewataka wanachama wa chama chake kuvunja makundi yaliyojitokeza wakati wa chaguzi wa ndani wa chama hicho.

“Vunjeni makundi chaguzi zimekiwasha tujikite kwenye kukiimarisha chama. CCM haitamvumilia mtu mwenye kuendeleza makundi,” amesema

Pamoja na hayo Dkt. Magufuli ameweka wazi hatosita kutengua matokeo ya uchaguzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu iwapo itabainika rushwa imetumika.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: