Chadema imepitisha wagombea 16  wa udiwani katika uchaguzi mdogo wa madiwani utakaofanyika Novemba 26,2017.


Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa amesema wagombea hao wameshapitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Amesema katika Kata ya Murieti iliyopo jimbo la Arusha Mjini aliyepitishwa ni Simon Mollel na Kata ya Moita, jimboni Monduli aliyeteuliwa ni Lobolu Lerango.

Golugwa amesema katika Kata ya Musa  iliyopo Halmashauri ya Arusha aliyepitishwa ni Elihud Laizer.

Katika Halmashauri Meru, amesema waliopitishwa na kata zao zikiwa kwenye mabano ni Dominick Mollel (Ambureni), Joyce Ruto (Makiba), Asantaeli Mbise (Maroroni), Daniel Mbise (Leguruki) na Emmanuel Salewa (Ngabobo).

Katika Jimbo la Hai, waliopitishwa ni Elibariki Lema (Machame Magharibi),  Moses Kalage (Weruweru), Ezra Ngapi (Mnadani) na Heldak Minde (Bomambuzi).

Amesema mkoani Tanga, aliyepitishwa ni Josiah Shemeta (Lugusa) na Jafari (Ndege Momba).

Kata ya Majengo wilayani Korogwe aliyepitishwa ni Abdallah Maoga na katika

 Kata ya Nangwa wilaya Babati aliyepitishwa ni Yohana Dafi.

Akizungumza uchaguzi huo, Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amesema wamejipanga kurejesha kata zote tano katika jimbo lake.

"Tumejipanga kufanya kampeni za kistaarabu na tuna uhakika wa ushindi," amesema.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: