MWALIMU Mkuu wa Shule ya Mtende, Mkoa wa Kusini Unguja anayetuhumiwa kumbaka mwanafunzi wa kidato cha nne amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa tuhuma hizo


Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja, Idrissa Kitwana Mustafa, alisema ofisi yake imeiandikia barua Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, ikiarifu hatua ya kumsimamisha kazi mwalimu huyo.

Alisema hatua hiyo inalenga kuwazindua walimu wengine wenye tabia za kudhalilisha wanafunzi kuacha mara moja.

Alisema inashangaza mwalimu kujihusisha na vitendo vya ubakaji wakati jamii inamtegemea kama ni mlezi wa watoto.

Alisema vitendo hivyo ni kinyume na maadili ya ualimu na havikubaliki kisheria hivyo alitaka jamii kuacha kuvifumbia macho.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: