SERIKALI imetenga Sh. bilioni 10 katika mwaka wa fedha 2017/18 kuwezesha upatikanaji wa dawa za kuzuia magonjwa nyemelezi.


Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa nchini (MSD), Laurean Bwanakunu, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utendaji wa bohari hiyo kwa kamati ya Bunge ya masuala ya Ukimwi.

Alisema hatua hiyo ya serikali imetokana na changamoto ya upatikanaji wa dawa hizo katika mwaka uliopita wa fedha kutokana na ufinyu wa bajeti ya serikali baada ya wafadhili kujitoa kununua dawa hizo.

“Serikali imetenga Sh. bilioni 10 ili kuwezesha upatikanaji wa dawa hizo na zitanunuliwa punde mgawo wa fedha utakapopatikana, hili limeenda sambamba na kuongeza ununuzi wa dawa za kawaida ambazo pia hutumia kwa kutibu magonjwa nyemelezi,”alisema Bwanakunu.

Aidha, alisema hali ya upatikanaji wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya Ukimwi(ARVs) ni asilimia 100.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: