Vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba imeendelea kujifua visiwani Zanzibar ikijiandaa na mchezo wake dhidi ya watani zao wa jadi Yanga itakayochezwa Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.


Jumla ya wachezaji 24 wa Simba pamoja na viongozi wao wamewasili Unguja asubuhi ya jana na jioni kuanza mazoezi kwenye Uwanaj wa Jeshini Migombani Mjini Unguja

 Simba itaendelea kufanya mazoezi kila siku asubuhi kuanzia saa 3:00 kwenye Uwanja wa Amaan na saa 10:00 za jioni katika Uwanja wa Jeshini Migombani.

Kikosi hicho kinachonolewa na Mcameroon Joseph Omog pamoja na msaidizi wake mpya Mrundi Masoud Djuma Irambona kimefikia kwenye Hoteli ya Mtoni Marine iliyopo Maruhubi Mjini Unguja.

Mshindi wa mechi hiyo ya watani wa jadi atajihakikishia kukalia usukani wa ligi baada ya timu hizo kulingana kwa pointi na kutofautiana kwa mabao.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: