
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Elexander Mnyeti jana amechaguliwa kuwa mmoja wa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM akiwakilisha wilaya ya kichama ya CCM ya Meru.
Mnyeti ambaye katika siku za karibuni, ameingia katika mgogoro na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akimtuhumu kuongoza njama za kuwanunua madiwani wa Chadema, alishinda baada ya kupata kura 266 akiwa hayupo ukumbini.
Katika nafasi hiyo ambayo ilikuwa inagombewa na wanaCCM 22, wajumbe wengine waliochaguliwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha(AICC), Elishilia Kaaya aliyepata kura 258 na Dk Daniel Mirisho alipata kura 327.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, uliofanyika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Makumira, mwenyekiti wa jumuiya ya wanawake wilaya ya Arusha, Mary Kisaka amesema katika nafasi hiyo, waliopiga kura walikuwa 586 kura zilizoharibika zilikuwa 3 na kura halali 583.
Katika nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya Meru, mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Andew Mungure aliweza kutetea kiti hicho baada ya kuwabwaga wagombea wenzake wawili.
Mungure alipata kura 471 na kuwabwaga Nevangirwa Mmari aliyepata kura 106 na Daniel Kaaya aliyepata kura 28.
Katika uchaguzi huo, Mbwana Hungura alichaguliwa kuwa katibu wa itikadi na uenezi wa wilaya hiyo baada ya kupata kura 50 na kuwashinda wanaCCM wengine wane ambapo kura halali zilikuwa ni 97
Post A Comment: