Aliyekuwa Msemaji wa Yanga SC, Jerry Muro amesema kutokana na uwezo wake katika mambo mbali mbali anaweza kujilinganisha na wabunge 10 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


Katika mahojiano na kipindi cha Maisha Mseto cha Times Fm, Jerry amesema kutokana na uwezo wake suala la ubunge kwake ni jambo rahisi tu sawa na kubofya button.

β€œMimi Jerry Muro mmoja ni sawa na wabunge 10 wa Chadema, nimewazidi kifikra, kinguvu, kipesa, maadili, kihoja na mambo mengine mengi sana” amese Jerry.

Katika hatua nyingine Jerry amesema mwaka 2020 si ajabu kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Edward Lowassa wakirejea katika Chama cha Mapinduzi (CCM).
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: