
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
MWENYEKITI wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Reginald Mengi, amempongeza Rais John Magufuli kwa ujasiri anaoendelea nao wa kupambana na rushwa na ufisadi huku pia akiipeleka Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Dk. Mengi aliyasema hayo jana mjini Bagamoyo, Pwani wakati alipotembelea eneo maalum la uwekezaji la KAMAL, ambapo pamoja na mambo mengine, aliwataka wawekezaji kuchangamkia maeneo hayo ambayo tayari yana miundombinu ya viwanda.
Alisema maeneo kama hayo ndiyo yatakayoharakisha kasi ya Rais Magufuli katika kuliwezesha taifa kufikia lengo la kuwa la uchumi wa viwanda.
Katika ziara hiyo, Dk. Mengi alipata fursa ya kujionea miundombinu iliyomo ndani ya eneo hilo la uwekezaji ambalo lina uwezo wa kujengwa viwanda hadi 100.
Akizungumza baada ya kutembelea eneo hilo, ndipo Dk. Mengi alipompongeza Rais Magufuli na serikali yake.
Alisema katika kipindi chake kifupi tangu aingie madarakani, amefanya mambo mengi makubwa yenye manufaa katika kukuza biashara na kwamba, TPSF inampongeza kwa ujasiri wake wa kupiga vita rushwa huku pia akisimamia kwa ukamilifu suala la ujenzi wa viwanda.
“TPSF inamuunga mkono Rais Magufuli kwa mambo haya mawili makubwa kupiga vita rushwa na suala la viwanda. Yapo mengine mengi amefanya katika maeneo kama vile elimu bure… tunampongeza,” alisema.
Kuhusu eneo hilo la uwekezaji, Dk. Mengi alisema ni muda mwafaka kwa wawekezaji kuchangamkia maeneo hayo ambayo tayari yana miundombinu ili kwenda na kasi ya Rais ya kuifikisha nchi kwenye uchumi wa viwanda.
“Viwanda vingi vimejengwa jijini Dar es Salaam ambako unakuta hapa kiwanda pale gesti au makazi ya watu. Maeneo kama haya ambayo yametengwa kwa ajili ya viwanda ndiyo yanatakiwa kuchangamkiwa kwa sasa,” alisema.
Dk. Mengi alisema eneo hilo liko tayari kwa ajili ya viwanda na hivyo wale waliokuwa wanauliza wakajenge wapi viwanda, sasa wanapaswa kuchangamkia fursa hiyo.
Pia alilitaka Shirika la Umeme (Tanesco) kuhakikisha wanakwenda sambamba na kasi ya Rais Magufuli kuhusu viwanda kwa kutoa kipaumbele kwa maeneo kama hayo ambayo viwanda vikubwa vitajengwa na kukuza uchumi wa nchi.
“Eneo kama hili linahitaji kuwa na umeme kwa ajili ya viwanda. Watu wengi hawamwelewi Rais vizuri… lakini anachosema ni muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu. Ni kweli nchi haiwezi kupiga hatua bila viwanda,” alisema.
Aidha, Dk. Mengi alimpongeza pia Mwenyekiti wa kampuni za Kamal, Gagan Gupta, kwa ushupavu wake wa kuona mbali na kuwekeza eneo hilo, ingawa wapo ambao hawakumwelewa hapo kabla nakumcheka.
“Alichekwa lakini leo yuko hapa na nina imani wanaotaka viwanda watakuja hapa na umeme utakuja. Nakushukuru kwa kuiamini Tanzania na kuja kuwekeza,” alisema.
Mwenyekiti wa kampuni za Kamal, Gupta, alisema eneo hilo lina ekari 285 ambazo zimekamilika tangu mwaka 2014, hivyo linafaa kwa uwekezaji kwa sababu lina miundombinu yote ikiwamo maji na barabara ya changarawe ya urefu wa kilomita saba ndani yake.
Pia alisema eneo hilo limegawanywa katika viwanja 280, ambavyo vinaweza kujengwa viwanda vikubwa na vidogo.
“Changamoto mbili ambazo zinahitaji ufumbuzi wa haraka ni laini ya umeme wa viwandani… tayari tumeshaongea na Tanesco na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDS) kwa ajili ya gesi asilia,” alisema.
Post A Comment: