Beki wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Banda (22) anayeichezea Baroka FC ya Afrika Kusini amethibisha kuwa huenda akajiunga na moja ya timu kubwa nchini humo.


Beki huyo wa zamani wa Simba alizitaja timu hizo kuwa ni SuperSport United FC ya Johannesburg na Kaizer Chiefs FC  ya Pretoria kuwa ni timu zinazopigana vikumbo kuwania saini yake.

β€œKule tunaongoza Ligi, wakati nafika na sasa mambo yako tofauti kwa sababu  ni kama nimekuwa mzoefu  kwa sababu nimecheza michezo yote saba ya Ligi Kuu,”

β€œKuna kila dalili kwamba sitacheza kwa muda marefu Baroka maana Kaizer Chiefs na SuperSport United zote zinanihitaji, sio rahisi kukataa aina hiyo ya madili, hizo ni timu kubwa ambazo kila mchezaji kwa huku anatamani kuzichezea.” alisema Banda.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: