Klabu ya Borussia Dortmund , imeushangaza ulimwengu wa soka baada ya kutangaza kumfukuza kazi kocha wake, Peter Bosz na kumuajili Peter Stöger.


Peter Bosz amepoteza michezo 12 tangu ajiunge na klabu hiyo na kitu pekee cha kushangaza ni kwamba Dortmund wamemuajili kocha ambaye ametimuliwa na klabu ya inayoshika mkia wa ligi kuu nchini Ujerumani Bundesliga.

Kuchaguliwa kwa Peter  Stöger kumezua gumzo kubwa nchini Ujerumani kwani wadau wengi wa soka wanasema Dortmund wamekosea kumsajili Kocha ambaye mwenye historia mbaya kwenye kufundisha timu za Ujerumani.

Peter Stoger amepoteza mechi 8 na kupata sare 3 kabla ya kutimuliwa na klabu ya FC Cologne ambayo inashika mkia kwenye msimamo wa Bundesliga. Ambapo imeelezwa kuwa ndio kocha wa kwanza kuanza vibaya kwenye tangu ligi hiyo ianzishwe.

Na hii inakuwa ni hatua ya kwanza kwenye historia ya Ligi kuu nchini Ujerumani kwa kocha mwenye karba hiyo kuajiliwa na klabu kubwa nchini humo.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: