
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
HATIMAYE wale wote walionufaika na mabilioni ya fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow ikiwa ni pamoja na kuzibeba siku moja kwa sandarusi, wako mbioni kutambulika majina yao na mwishowe kufikishwa mbele ya mkono wa sheria.
Aidha, kibano kama hicho kimewadia pia kwa vigogo walioficha mabilioni ya fedha katika akaunti za siri ughaibuni, ikiwamo Uswisi barani Ulaya.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kamishna wa Polisi Valentino Mlowola, ndiye aliyefichua jambo hilo jana katika mkutano wa mwaka wa viongozi wa Takukuru uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mlowola hakuwataja moja kwa moja wahusika wa kashfa ya uchotwaji wa fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow na pia wa mabilioni ya Uswisi.
Hata hivyo, aligusia hesabu zao za kuwatia pingu wahusika kwa kusisitiza kuwa wanaelekeza nguvu katika kushughulikia uchunguzi wa kashfa kubwa nchini ili fedha za umma zirejeshwe serikalini na sheria kutwaa mkondo wake pasi na kumwonea mtu wala kumwacha kwa sababu ya nafasi yake katika jamii.
Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ambaye alikuwa akijibu swali la papo kwa papo kuelekea kwake lililoulizwa Mei 11 mwaka huu na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, kashfa kubwa za rushwa ni pamoja na Akaunti ya Tegeta Escrow, mabilioni ya Uswisi na Operesheni Tokomeza.
Aidha, katika mijadala ya Bunge kuhusu ripoti ya kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow iliyohusisha uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300, ilielezwa kuwa kuna siku, wakati wa uchotwaji wa fedha hizo, baadhi ya wanufaika walibeba noti za mabilioni ya fedha kwa mifuko ya sandarusi baada ya kuyatoa kwa mkupuyo kutoka benki.
Aidha, ilielezwa kuwa majina ya baadhi ya wanufaika wa katika uchotwaji wa fedha hizo hayakuwa yakifahamika.
KIBANO TAKUKURU
Akifafanua jana kuhusiana na dhamira yao ya kuhakikisha kuwa fedha zote za umma zilizotwaliwa na baadhi ya watu katika rushwa kubwa zinarejea mikononi mwa serikali, Kamishna Mlowola alisema uchunguzi wa kashfa kubwa utapewa kipaumbele zaidi na kukamilishwa kwa wakati.
Aliongeza kuwa Takukuru itafanikisha jambo hilo kwa kuwakamata na kuwachunguza watuhumiwa kwa kuzingatia sheria, pasi na kumuonea mtu wala kujali nafasi aliyonayo.
“Kama nilivyotoa tahadhari mwanzoni mwa mwaka 2016, kwamba yeyote atakayehujumu au kuiba mapato ya serikali hatobaki salama, bila kujali aliyaiba lini mapato hayo,” alisema Kamishna Mlowola na kuongeza:
“Narudia tena kutoa onyo na tahadhari kwa waliozoea kufanikiwa kwa njia zisizo halali na rushwa kwamba Takukuru haitowaacha salama. Tutawashughulikia bila huruma kwa mujibu wa sheria zinazotuongoza kutekeleza wajibu wetu… kama Rais alivyotangaza vita dhidi ya rushwa.”
Alisema katika kipindi cha 2016/2017, Takukuru ilifanikiwa kuokoa kiasi cha fedha zaidi ya Sh. bilioni 14. Pia imefanikiwa kuimarisha zaidi mifumo ya utoaji huduma kwa wananchi, pamoja na eneo la uelimishaji umma.
Tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani Novemba 5, 2015, kasi ya mapambano dhidi ya rushwa imeongezeka kwa kasi na hadi sasa, tayari Takukuru, chini ya Kamishna Mlowola, imefanikisha kufikishwa kortini kwa watuhumiwa wa makosa mbalimbali yanayohusiana na rushwa, uhujumu uchumi na utakatishaji fedha.
Post A Comment: