
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
FAMILIA ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, imeitaka serikali kuruhusu wapelelezi wa kimataifa kuchunguza tukio la kujeruhiwa kwa risasi kwa mwanasiasa huyo "ili haki itendeke".
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, kaka wa Lissu, Alutes Mughwai, alisema Waziri wa Katiba na Sheria na Mwanasheria Mkuu wa serikali wamepokea barua ya familia ya kutaka wapelelezi wa nje na kwamba majibu yake yatatolewa atakaporudi nyumbani kwake Arusha.
"Tunataka kuona upelelezi wa kina, haraka na kitaalamu ili waovu wajulikane na kukamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa Sheria," alisema Mughwai.
"Kwenye barua yetu tumependekeza kuwa serikali ishirikishe watalaamu wa uchunguzi kutoka nje ili kuwa na uchunguzi huru wa kuridhisha pande zote."
Aidha, Mughwai ambaye ni wakili wa kujitegemea alisema uchunguzi wa kimataifa unawezekana kwa kuwa kuna sheria ya ushirikiano katika mambo ya jinai, na Tanzania ni sehemu ya jumuiya ya kimataifa.
Alisema kuja kwa wapelelezi kutoka nje haitakuwa mara ya kwanza kufanyika katika tukio la Lissu kwani mwaka 1984 wakati jengo la Benki Kuu (BoT) lilipoungua, wataalamu hao walikuja.
Aidha alisema mwaka 1998 Ofisi za Ubalozi wa Marekani nchini zilipolipuliwa kwa bomu serikali iliomba wapelelezi kutoka nje.
Hata hivyo, kwa kuwa ubalozi ni nchi ya kigeni kisheria, Marekani ilikuwa na uwezo wa kutumia makachero wake wa mashirika ya FBI na CIA.
Akizungumzia matakwa ya polisi kwamba dereva wa Lissu aliyeko na majeruhi Nairobi arudi kwa mahojiano, Mughwai alisema familia inaona usalama wake uko matatani kwa kuwa hadi sasa waliommininia risasi Lissu hawajakamatwa na dereva huyo hajahakikishiwa usalama.
"Polisi wamesimamisha upelelezi kwa sababu mtu mmoja hajarudi, tuna Ubalozi Nairobi kwanini wasimfuate huko?" Aluliza.
"Angekuwa amejeruhiwa yuko hospitali asingehojiwa? Badala ya kusubiri arudi (wamfuate)."
Aidha, alisema katika eneo la tukio hakuwapo dereva huyo pekee bali pia walinzi wa nyumba za viongozi wengine.
"Hatuko tayari jambo hili kufanywa siasa na Lissu wanamfanya kama mpira wa kona, sisi (familia) kuwa wabeba vibendera.
"Tunataka apone, jambo lake lichunguzwe vizuri na ukweli ujulikane."
Lissu alishambuliwa kwa risasi 32 nje ya nyumba yake Septemba 7 mjini Dodoma, majira ya mchana na watu wasiojulikana.
Katika shambulio hilo ambalo limelaaniwa na watu wengi wa ndani na nje ya nchi, Lissu alivunjika mguu wa kulia, mkono wa kushoto na nyonga na ameshafanyiwa operesheni kadhaa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na Hospitali ya Nairobi alikolazwa sasa.
Baada ya tukio hilo, Lissu (49), aliwahishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ambako alipatiwa matibabu ya awali kabla ya kusafirishwa kwenda Kenya kwa ajili ya matibabu zaidi.
Taarifa za awali zinadai watu waliompiga risasi walikuwa wakimfuatilia kutoka bungeni, na kwamba walikuwa wakitumia gari nyeupe aina ya Nissan Patrol.
Hadi sasa polisi haijamkamata mtu yeyote kuhusiana na shambulio hilo.
Post A Comment: