Katika Mkutano wa Saba wa Bunge la Kumi na unaoanza leo kamati mbili zilizoundwa na Spika John Ndugai kuhusu madini ya tanzanite na almasi zitawasilisha ripoti zao.


Taafifa iliyotolewa na ofisi ya Bunge jana Jumatatu imeeleza kuwa kamati hizo zilizopewa siku 30 zimekamilisha kazi

hiyo na zitawasilisha taarifa zao keshokutwa tarehe 6 Septemba 2017 katika hafla fupi itakayofanyika katika viwanja vya Bunge na kuhudhuriwa na viongozi wa kitaifa.

Katika tukio hilo imeelezwa Spika atapokea taarifa hizo na kuzikabidhi kwa Waziri Mkuu.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: