Rais Uhuru Kenyatta ametetea hatua yake ya kuikosoa mahakama ya juu na Jaji Mkuu David Maraga kwa kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa urais akisema ni haki yake kufanya hivyo.


Akizungumza katika kampeni za chama cha Jubilee katika kaunti ya Kajiado leo, Rais Kenyatta amesisitiza madai yake kwamba mahakama hiyo ya juu ilipuuzia mbali haki ya wananchi ili 'kumfurahisha' mtu mmoja aliyemtaja kuwa mpinzani wake Raila Odinga.

Amesema, licha ya kuwa anaheshimu uamuzi wa mahakama hiyo anajua kwamba alishinda uchaguzi huo kwa zaidi ya kura milioni 1.4. na kwamba, ana imani atashinda tena uchaguzi wa marudio.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: