Wanafunzi 917,072 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi kesho na kesho kutwa [Septemba 6 na 7], huku kati ya wanafunzi hao, wasichana ni 484,328 sawa na asilimia 52.81 huku wavulana wakiwa ni 432,744 sawa na asilimia 47.19,.


Watahiniwa 882,249 watafanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili na 34,823 watatumia lugha ya Kiingereza.

Katibu Mtendaji wa baraza la mitihani Dk Charles Msonde amesema maandalizi kwaajili ya mitihani huo umekamilika ikiwa ni pamoja na kusambaza karatasi za mitihani, fomu maalumu za kujibia mitihani na nyaraka zote muhimu kwaajili ya mtihani huo.

Aidha Msonde ametoa onyokali kwa wasimamizi wa mitihani, waalimu, wananchi na wamiliki wa shule watakao jaribu kufanya udanganyifu kuwa watachukuliwa hatua ikiwa pamoja na kufungia shule zote zitakazofanya udanganyifu.

Jumla ya watahiniwa 94 wasioona wamesajiliwa kufanya mtihani huo, wakiwemo wavulana 58 na wasichana 36, Dk Msonde amezitaka halmashauri kuhakikisha utaratibu wa uendeshaji wa mitihani unazingatiwa.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: