Wabunge wa kambi rasmi ya upinzani bungeni wamegomea shughuli za kiapo cha wabunge wateule wa Chama cha wananchi (CUF) ili kuwaunga mkono wabunge waliovuliwa uanachama na kupoteza ubunge pamoja na kupinga bunge kutumika na serikali kukandamizi upinzani.


Wakizungumza katika viwanja vya Bunge, huku wabunge wateule wakiendelea kuapishwa ndani ya Bunge, Katibu wa Kambi rasmi ya upinzani bungeni Mhe David Silende amesema kambi rasmi ya upinzani haitawapa ushirikiano wabunge hao mpaka kesi ya msingi itakapo malizika mahakamani.

Kwa upande wake Katibu wa Bunge wa Chama cha wananchi (CUF), Juma Kombo Hamad amesema vyama vya upinzania vinadai haki itendeke katika masuala yote ya msingi na kusisitiza kinacholalamikiwa ni kufukuzwa kwa wabunge katika chama ambacho kina mgogoro haukufuata misingi ya sheria na Katiba.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: