KUPITIA albamu yake ya kimataifa inayoitwa A Boy From Tandale, msanii Abdul Naseeb ‘Diamond Platnumz’ amefanikiwa kumnasa na kumshirikisha mcheza ‘violin’ maarufu raia wa Israel na Marekani, Miri Ben Ari, katika wimbo wa Baila, utakaopatikana kwenye albamu hiyo.
Mrembo huyo mshindi wa tuzo kubwa ya Grammy, ambaye aliwahi kuitwa kutumbuiza Ikulu ya Marekani na Rais mstaafu Barack Obama na kufanikiwa kufanya kazi na wasanii nyota duniani kama Jay Z, Alicia Keys, Kanye West, Janet Jackson, T Pain na Twista, ameonjesha kionjo cha ufundi alioufanya kwenye wimbo wa Diamond Platnumz kupitia Instagram yake na kusema:
“Shukrani na pongezi nyingi kwa rafiki yangu mwenye vipaji vingi, Diamond Platnumz kwa albamu yako mpya, naupenda huu wimbo, Baila tumefanya pamoja na tunatazamia kuja kuutumbuiza pamoja, amani na baraka,” aliandika mrembo huyo kwa lugha ya Kiingereza.
Post A Comment: