BEKI wa zamani, Jamie Carragher, ameingilia kati mvutano unaoendelea kati ya klabu yake ya zamani ya Liverpool na Barcelona juu ya nyota Philippe Coutinho.


Barca wameendelea kung’ang’ania mpango wao wa kumsajili Mbrazil huyo ingawa wameshaambiwa na mabosi wa Anfield kwamba hauzwi kwa kiasi chochote cha fedha.

Kwa upande wake, mkongwe Carragher, ambaye alikuwa kwenye kikosi cha Liver kilichotwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2006, amesema kuuzwa kwa Coutinho si tatizo kama ambavyo ingekuwa kwa Sadio Mane.

Mkongwe huyo amedai kuwa Mane ana umuhimu mkubwa kikosini kuliko Coutinho.

“Najua nitatengeneza mjadala mkubwa kutokana na falsafa ya Jurgen Klopp, lakini nafikiri Mane ni muhimu zaidi kwenye kikosi cha Liverpool,” alisema Carragher.

Mane aliifungia Liver bao la ushindi dhidi ya Crystal Palace kwenye mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa msimu huu uliochezwa kwenye Uwnaja wa Anfield, ambapo Coutinho aliukosa mtanange huo kutokana na maumivu ya mgongo.

Carragher anaamini Msenegal huyo ndiye aliyekuwa moto wa kuotea mbali msimu uliopita na kuisaidia Liver kumaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

“Angalia anafunga mabao yake, jinsi yalivyo muhimu kwenye timu tangu alipojiunga na timu hiyo. Ni mchezaji wa pembeni sawa, lakini ana idadi kubwa ya mabao akikimbizana na washambuliaji,” alisema Carragher.

“Kama tutamlinganisha na Coutinho anayetakiwa na Barcelona, bado Mane ana sababu ya kutembea kifua mbele. Akiendelea kwa kasi ile na kiwango kile basi atazivutia timu kubwa zaidi barani Ulaya.”

Hata hivyo, Carragher anaamini kwamba, Coutinho hataondoka Liver licha ya Barca kumkalia kooni wakimtaka kuziba pengo la Neymar.

“Bado wataendelea kumng’ang’ania kwa sababu ni moja ya wachezaji muhimu kwenye klabu. Sioni kama ni vibaya kumbakiza kwa wakati huu,” alisema.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: