Beki mpya wa Simba, Erasto Nyoni ameanza kufuata nyayo za beki mwingine wa timu hiyo, Shomari Kapombe katika kutupia mabao.


Kapombe ndiye beki alifunga mabao mengi katika miaka ya karibuni ambapo alifunga mabao manane Ligi Kuu msimu wa 2015/16.

Hata hivyo Nyoni ambaye ametua Simba msimu huu, ameanza kuweka rekodi ya aina yake baada ya kufunga mabao manne katika mechi nane alizocheza hivi karibuni.

Nyoni alianza kwa kufunga bao safi kwenye mchezo wa Taifa Stars na Zambia katika michuano ya COSAFA kabla ya kufunga tena katika mchezo wa kirafiki kati ya Bidvest Wits ya Afrika Kusini na Simba.

Beki huyo anayemudu kucheza nafasi zote za ulinzi, alifunga pia dhidi ya Gulioni ya Zanzibar kabla ya kufunga tena dhidi ya Ruvu Shooting juzi Jumamosi hivyo kuwa beki wa Simba aliyecheka na nyavu zaidi.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: