
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
RAIS John Magufuli ameamuru kurudishwa serikalini kwa viwanda vyote vya umma vya zamani ambavyo viliuzwa kwa wawekezaji binafsi miaka ya 1990 lakini vikatelekezwa au kubadilishwa matumizi yake.
Rais alitoa agizo hilo akiwa ziarani mkoani Pwani juzi, taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu imesema.
Akiwa katika siku ya mwisho ya ziara hiyo, Rais Magufuli alimuagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kuwanyang’anya viwanda watu wote waliouziwa viwanda na serikali na baadaye kuvitelekeza ili wapatiwe wawekezaji wengine wenye uwezo wa kuviendeleza.
Rais Magufuli alisema viwanda 197 viliuzwa kwa watu mbalimbali kwa lengo la kuviendeleza, taarifa hiyo ilisema, lakini baadhi vimekufa na vingine kubadilishiwa matumizi.
Rais alisema jambo hilo linarudisha nyuma juhudi za serikali ya awamu ya tano za kutekeleza mpango wa ujenzi wa viwanda, taarifa ya Ikulu ilieleza zaidi.
“Mheshimiwa Waziri, wale waliopewa viwanda miaka ile kwa kuuziwa bei ya chee, tukitegemea kwamba vile viwanda vitaendelea kufanya kazi lakini wamevitelekeza na vingine havipo kabisa, usiwe na kigugumizi na wala usiangalie sura, wanyang’anye," taarifa ya Ikulu ilimkariri Rais Magufuli akisema.
Taarifa hiyo ilisema Rais ameagiza vitega uchumi hivyo virudishwe serikalini ili wawekezaji wenye nia ya kujenga viwanda wapewe kwa sababu "kiwanda sio mwanamwali wa kumtunza ndani.
"Kinatakiwa kifanye kazi, kitoe ajira, na Serikali ipate mapato.”
Rais Magufuli alitoa agizo hilo baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha kusindika matunda cha Sayona Fruits kilichopo katika kijiji cha Mboga, wilayani Bagamoyo, kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu.
Kitakapokamilika, kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kusindika tani 300 za matunda mbalimbali kwa siku, kuajiri wafanyakazi 800 na kunufaisha wakulima 30,000 mkoani Pwani.
Taarifa ilisema kiwanda hicho kinajengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh. bilioni 120.
Serikali ilibinafsisha mashirika ya umma, ikiwemo viwanda zaidi ya 300 katika serikali za awamu ya pili ya rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na awamu ya tatu ya Benjamin Mkapa baada ya kuonekana kwamba mashirika hayo yalikuwa ni mzigo kwa mlipa kodi.
AHADI ZA 2015
Urejeshaji serikalini viwanda vilivyokufa baada ya kubinafsishwa ni moja ya ahadi za Rais Magufuli wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Aidha, akijibu swali bungeni Septemba 14, mwaka jana, Waziri Mwijage alisema Serikali imekuwa ikitekeleza agizo la Rais Magufuli la kuhakikisha viwanda vilivyobinafsishwa vinafanya kazi tangu Novemba, 2015 ikiwa ni mwezi ambao aliapishwa.
Mwijage alisema hilo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Manyoni, Yahaya Massare lililohusu utekelezaji wa ahadi ya Rais kurudisha viwanda vyote vilivyobinafsishwa lakini havifanyi kazi.
Waziri Mwijage alisema Serikali kupitia wizara yake ilikuwa ikiendelea na zoezi la kuchambua mikataba ya mauzo kwa viwanda vilivyobinafsishwa ambavyo ama havifanyi vizuri au vimesimamisha uzalishaji kabisa.
Waziri alibainisha kuwa timu ya wataalamu toka Wizara ya Viwanda na Ofisi ya Usajili wa Hazina walifuatilia na kufanya tathimini kwa kutembelea kiwanda baada ya kiwanda.
Aidha, Waziri Mwijage alisema uchambuzi wa mikataba ya viwanda hivyo ulikuwa ukifanyika kwa ushirikiano na Ofisi ya Msajili wa Hazina na wizara za kisekta ikiwamo Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Nishati na Madini, pamoja na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Na sasa Rais Magufuli ameagiza kuwanyang’anya viwanda watu wote waliouziwa viwanda na serikali na baadaye kuvitelekeza ili wapatiwe wawekezaji wengine wenye uwezo wa kuviendeleza.
Post A Comment: