Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mtoto wa miaka miwili Buyunga Baragi amekutwa akiwa amechinjwa, huku panga lenye matone ya damu likiwa ndani ya nyumba anayoishi. 


Mtoto huyo, mkazi wa Kijiji cha Iharara, wilayani hapa Mkoa wa Mara, alichinjwa akiwa amelala chumbani pamoja na watoto wenzake. 

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho, Makuru Siboti alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 12 :30 jioni na kuibua hofu na simanzi miongoni mwa wakazi wa eneo hilo. 

Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Serengeti, Alfred Kyeba aliyeongoza kikosi cha uchunguzi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. 

Akizungumza kifo cha mjukuu wake, Bendu Baragi alisema tukio hilo liligundulika baada ya wazazi kurejea nyumbani kutoka kwenye shughuli zao za kila siku. 

Baragi alisema aliyebaini mauaji hayo ni mama wa marehemu, Silya Fadhili aliyekuwa ametoka kuchunga mifugo yake na kuwakuta watoto wake wamelala lakini alipowaangalia vizuri aligundua mmoja wao alikatwa shingo. 

"Polisi wamefika hapa nyumbani na kuondoka na baba wa marehemu pamoja na shangazi yake baada ya panga lenye matone ya damu kukutwa ndani ya nyumba ya familia", alisema Baragi. 

Hili ni tukio la pili la mtu kuuawa kwa kuchinjwa wilayani Serengeti, likitanguliwa na lile mkazi wa Kitongoji cha Mariwa, Kijiji cha Nyiberekera, Teksi Ngiteli (21), aliyekutwa amechinjwa nyumbani kwao.

Chanzo: Mwananchi
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: