w1

Simba imeendelea kujichimbia kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya JKT Ruvu mchezo uliomalizika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.


Timu ya wanajeshi hao miongoni mwa timu tatu zilizo kwenye mstari wa kushuka daraja pamoja na Toto African na Majimaji dakika ya 42 kiungo mahiri Mzamiru Yassin aliwapa furaha mashabiki wa Simba baada ya kufunga goli akiunganisha krosi ya Paschal Athanas.

Kipindi cha pili hakuna timu iliyoweza kupata goli licha ya kufanya mabadiliko mbalimbali hadi mwamuzi anamaliza mpira Simba wameibuka na ushindi wa goli 1-0 na ukiwa mchezo wa pili kwa kocha Bakari Shime kupoteza mechi tangu aichukue timu hiyo.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kuendelea kutesa kileleni mwa ligi ikifikisha pointi 41, alama nne zaidi ya wapinzani wao Yanga wenye pointi 38 wakiwa nafasi ya pili.
DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: