KIUNGO na aliyewahi kuwa nahodha wa Simba, Jonas Mkude amewataka wachezaji wenzake kutambua thamani ya kuvaa jezi ya Simba kwa kuhakikisha wanaipigania mpaka wabebe ndoo haswa kutokana na uwekezaji wa Mohammed Dewji ‘MO’.
Simba inaongoza msimamo wa ligi kuu kwa kuwa na pointi 23, sawa na Azam FC wakipishana idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Mkude ambaye anasimamiwa na meneja, Richard Kiwale, alisema kuwa, kutokana na klabu hiyo kuingia katika mabadiliko ya kimfumo kwa timu kukabidhiwa kwa MO kuna kila sababu ya wachezaji kutambua thamani ya jezi zao.
“MO ni mtu sahihi Simba, niipongeze klabu kuweza kumpatia timu, ni mtu mwenye mapenzi ya dhati ya kuifikisha Simba mbali. Hivyo kutokana na uwepo wake ni vyema kwa wachezaji wajitolee na kucheza kwa moyo wote pia kujua umuhimu na thamani ya jezi ya Simba ili kutwaa ubingwa msimu huu,” alisema Mkude ambaye kabla msimu haujaanza alihusishwa kutaka kujiunga na Yanga.
Post A Comment: